1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS: Mkutano muhimu wa viongozi wa Afrika Kaskazini uliotarajiwa ...

22 Desemba 2003

mjini Algiers Jumaane na Jumaatano umeahirishwa kwa ajili ya kuibuka tafauti za kijimbo. Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafy alitarajiwa kuhudhuria mkutano huo kuzungumzia uzinduzi wa eneo huru la biashara. Umoja wa nchi za kiarabu wa Maghareb unazileta pamoja, Algeria, Libya, Mauritania, Morocco na Tunisia, na kwa jumla una wakaazi millioni 80. Umoja huo ulianzishwa mwaka 1989 ili ufanane na Muungano wa Ulaya, lakini haikuwezekana kwa sababu za tafauti za maoni kati ya Algeria na Morocco. Umoja umeingia tena matatani jana, pale Morocco ilipoarifu Mfalme Mohammed hatahudhuria kutokana na ugomvi kati ya Algeria na Morocco kuhusika na suala la Sahara Magharibi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW