1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS : Mkutano wa Waarabu wafunguliwa

22 Machi 2005

Mkutano wa siku mbili wa viongozi wa Waarabu umefunguliwa mjini Algiers Algeria leo hii kujadili agenda yenye vipengele 17 ikiwa ni pamoja na mpango wa amani Mashariki ya Kati.

Viongozi wa juu 13 kutoka nchi wanachama 22 wa Umoja wa Waarabu wameshiriki katika hafla ya ufunguzi wakati nchi nyengine zimepeleka wawakilishi waandamizi.Mkutano huo ulifunguliwa na Rais wa Tunisia Zine al Abidine Ben Ali mwenyekiti wa mkutano wa viongozi wa mwaka jana.

Duru zilizo karibu na mkutano huo zimesema viongozi hao watawasilisha mpango wenye kuipatia fursa Israel ya kurudisha uhusiano wa kawaida na nchi za Kiarabu ili nayo ijitowe kabisa kwenye ardhi iliyoiteka katika vita vya mwaka 1967.

Mkutano huo unafanyika sambamba na miaka 60 tokea kuundwa kwa Umoja huo wa Waarabu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW