1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS : Mripuko wa bomu umeua mmoja na kujeruhi 9

11 Desemba 2006

Shambulio la bomu lililofanywa dhidi ya basi lililopakia wafanyakazi wa kigeni,limemuua dreva wa basi hilo na kuwajeruhi wasafiri tisa.Miongoni mwa hao waliojeruhiwa ni Mmarekani mmoja,Mkanada na Waingereza wawili.Shambulio hilo limefanywa magharibi ya mji mkuu Algiers.Mashahidi wanasema milio ya risasi ilisikika baada ya mripuko wa bomu.Hadi hivi sasa,hakuna alietangaza kuhusika na shambulizi hilo.Wafanyakazi hao wameajiriwa na kampuni la Kimarekani na Kialgeria linalohusika na kampuni la Kimarekani Halliburton ambalo hushughulika na kazi za ujenzi na uhandisi katika sekta za mafuta na gesi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW