ALGIERS: Mwanamgambo ajiripua katikati ya umati
7 Septemba 2007Matangazo
Nchini Algeria,mshambulizi wa kujitolea maisha muhanga,ameua watu wasiopungua 15 na kuwajeruhi zaidi ya watu 70.Mshambulizi huyo alijiripua na bomu,katikati ya umati uliokuwa ukimngojea Rais Abdelaziz Bouteflika aliepanga kutembelea mji wa Batna,mashariki ya nchi.
Baadae Rais Bouteflika,alizungumza kwenye televisheni na kuwalaani wale waliohusika na shambulizi hilo.Akasema,ataendelea na mradi wake wa upatanisho wa kitaifa,ambao unatoa msamaha kwa wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali, waliojitenga na matumizi ya nguvu.