ALGIERS: Uchaguzi wa bunge nchini Algeria
17 Mei 2007Matangazo
Wapiga kura nchini Algeria hii leo wanachagua bunge jipya,chini ya ulinzi mkali wa usalama. Kuna hofu kuwa makundi yenye itikadi kali za Kiislamu huenda yakasababisha machafuko.Mwezi uliopita,katika mji mkuu Algiers,watu 30 waliuawa na wengine 220 walijerhiwa katika mashambulizi matatu ya kujitolea muhanga.Tawi la Al-Qaeda nchini Algeria,lilidai kuhusika na mashambulio hayo.Inatazamiwa kuwa serikali ya muungano wa vyama vitatu,chini ya uongozi wa chama cha FLN cha Rais Abdelaziz Bouteflika itashinda uchaguzi wa hii leo.