Algiers. Umoja wa mataifa walaani shambulio.
14 Aprili 2007Matangazo
Ulinzi umeendelea kuwa imara nchini Algeria , siku mbili baada ya mashambulio mawili ya mabomu katika mji mkuu Algiers kuuwa kiasi watu 33 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 200.
Katika taarifa kali, baraza la usalama la umoja wa mataifa limelaani shambulio hilo la Jumatano mjini Algiers na kudai kuwa wahusika wafikishwe mbele ya sheria.
Kundi linalojiita Al-Qaeda katika Maghreb, limedai kuhusika na shambulio hilo.