ALGIERS : Waalgeria waunga mkono msamaha wa waasi wa Kiislam
30 Septemba 2005Matangazo
Sehemu kubwa ya wananchi wa Algeria imeunga mkono msamaha wa kiasi fulani kwa mamia ya wanamgambo wa Kiislam kwa lengo la kukomesha muongo mmoja wa uasi uliouwa takriban watu 150,000 wengi wao wakiwa raia.
Lakini mashirika ya haki za binaadamu yanadai kwamba Rais Abdelaziz Bouteflika anaitumia kura hiyo ya maoni kwa mpango huo wa amani wa serikali kwa kujaribu pia kufuta uhalifu uliofanywa na vikosi vya usalama.Juu ya kwamba baadhi ya Waalgeria walizifukia kadi za kura kwenye makaburi ya watu wao waliopoteza maisha yao kutona na uasi huo wengi wamesem wako tayari kusamehe.
Asilimia 80 ya watu milioni 18 wa taifa hilo la Afrika kaskazini wameshiriki katika kura hiyo ya maoni hapo jana ambayo matokeo yake yatatangazwa leo hii.