1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS: Wanajeshi sita wa Algeria wauwawa

9 Aprili 2007

Wanajeshi sita wa Algeria na wanamgambo sita wa kiislamu wameuwawa kwenye mapigano magharibi mwa mji mkuu Algiers nchini Algeria.

Mapigano yalizuka Jumamsoi jioni baada ya msafara wa jeshi kushambuliwa katika eneo la msitu la Zaccar. Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na uvamizi huo lakini unafuatia harakati ya kijeshi dhidi ya kundi linalojiita kitengo cha jeshi cha kundi la Alqaeda katika eneo la kiislamu la Maghreb.

Algeria imekuwa ikikabiliana na upinzani mkali uliozuka mnamo mwaka wa 1992 wakati jeshi lilipofutilia mbali uchaguzi wa bunge ambao ulielekea kushindwa na chama cha kiislamu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW