1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS: Wanamgambo washambulia vikosi vya serikali

16 Mei 2005

Wanajeshi 12 wa Algeria wameuawa,katika shambulio la ghafla lililofanywa mwishoni mwa juma na waasi wa Kiislamu katika jimbo la mashariki la Khenchela.Vyombo vya habari vya Algeria vikiripoti habari hiyo vimesema,bomu liliripuka siku ya jumapili wakati msafara wa vikosi ulikuwa ukipita karibu na mji wa Khenchela,ulio kama kilomita 540 kusini ya mji mkuu Algiers.Kwa mujibu wa magazeti ya nchini humo,kikundi cha GSPC kinachodaiwa kuwa na mahusiano na Al-Qaeda ndio kimehusika na shambulio hilo.Katika kipindi cha wiki sita za nyuma,si chini ya watu 60 wameuawa nchini Algeria na zaidi ya nusu walikuwa askari wa usalama.Ripoti za maafisa na za vyombo vya habari zinawalaumu wanamgambo wa kiislamu kwa mashambulio hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW