1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS:Iran yasisitiza kuendelea na mpango wake wa nuklia

7 Agosti 2007

Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad amesema kuwa nchi yake itaendelea na mpango wake wa nishati ya nuklia na hawako tayari kuzungumza na nchi yoyote ambayo haithamini haki za nchi hiyo kuwa na matumizi ya kiraia ya nishati hiyo.

Akizungumza mjini Algiers Algeria Rais Ahmadnejad amesititiza kuwa watu wa Iran watendelea na mpango wake wa kuwa na nishati hiyo.

Nchi za magharibi zikiongozwa na Marekani zimekuwa zikitaka Iran kusitisha mpango wake huo zikisema ni njia ya kutengeza bomu la nuklia.

Tayari Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekwishaiwekea vikwazo Iran kwa kuendelea kugoma kusitisha urutubishaji wa madini ya Uranium