1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algiers.Watu 14 wauwawa nchini Algeria.

9 Aprili 2005

Idadi ya watu waliokufa kutokana na shambulio la kushtukiza lililofanywa na wapiganaji wa Kiislamu, ambao waliweka kizuwizi bandia cha barabarani karibu na mji wa Larbaa, kiasi cha kilometa 30 kusini mwa mji mkuu Algiers, imefikia 14.

Duru za kiusalama nchini Algeria zimeliambia shirika la habari la Ufaransa AFP leo kuwa mwili wa msichana mmoja ulipatikana katika eneo la milima karibu na eneo wapiganaji hao walipofanya shambulio lao dhidi ya magari manne, siku ya Alhamis, na kuyafyatulia risasi.

Jana maafisa wa usalama wamesema kuwa watu 13 wameuwawa na mtu mmoja amejeruhiwa. Shambulio hilo limekuja siku moja tu baada ya rais Abdelaziz Bouteflika kulihutubia taifa ambapo alidai kuwa hali ya usalama imerejeshwa kwa kiasi kikubwa kila mahali nchini humo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW