SiasaMarekani
Aliyevujisha nyaraka za siri Marekani afikishwa mahakamani
14 Aprili 2023Matangazo
Jack Teixeira mwenye umri wa miaka 21 na mfanyakazi wa kamandi ya kikosi cha ulinzi wa anga ya Marekani alikamatwa jana Alhamisi baada ya wiki nzima ya uchunguzi juu ya kuvuja kwa nyaraka nyingi za siri ikiwemo kuhusu vita vinavyoendelea nchini Ukraine.
Soma pia: Pentagon yamnasa mtu anayeshukiwa kuvujisha nyaraka za siri
Wizara ya Sheria ya Marekani inatazamiwa kuainisha kesi ya jinai inayomkabili na kumfungulia mashtaka chini ya sheria ya ujasusi inayoainisha kuwa ni kosa kuvujisha taarifa za ulinzi wa taifa
Waendesha mashtaka wanaamini kijana huyo ambaye pia ni mtaalamu wa teknolojia alikuwa kiongozi wa kundi la mawasiliano kwenye mtandao ambako nyaraka hizo za siri zilisambazwa.