Alonso ajiunga na Bayern kutoka Real Madrid
29 Agosti 2014Uhamisho wa mchezaji huyo Mhispania mwenye umri wa miaka 32 umekamilika jana na sasa anatarajiwa kulijaza pengo lililoachwa wazi na mhispania mwenzake Javi Martinez ambaye anauguza jeraha.
Alonso alijiunga Real Madrid kutokea Liverpool mwaka wa 2009, na akaisaidia kushinda taji la Ligi ya Mabingwa mwezi Mei mwaka jana baada ya Madrid kuwabandua nje mabingwa watetezi Bayern katika nusu fainali.
Madrid ilimsaini Toni Kroos kutoka Bayern msimu huu, pamoja na nyota wa Colombia James Rodriguez, na kuimarisha ushindani katika safu ya katikati. Alonso ni mchezaji wa pili muhimu kuwaambia kwaheri mabingwa hao wa Ulaya wiki hii baada ya Angel Di Maria kujiunga na Manchester United.
Kwingineko, Borussia Dortmund wanakaribia kumsaini tena kiungo Mjapan Shinji Kagawa baada ya kuwa na miaka miwili yene matatizo chungu nzima katika klabu ya Manchester United.
Ripoti za yombo vya habari Uingeraza na Ujerumani zinasema kuwa mazungumzo baina ya timu hizo mbili yamepiga hatua kubwa. Kipindi cha usajili wa wachezaji kinakamilika Jumatatu wiki ijayo.
Kagawa mwenye umri wa miaka 25 alipendwa saan na mashabiki wa Dortmund ambayo aliichezea kuanzia mwaka wa 2010 hadi 2012 na kushinda Bundelsiga mwaka wa 2011 na kombe la SHirikisho la Soka Ujerumani – DFB mara mbili. Alifunga magoli 21 katika mechi 49 za Bundesliga.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu