1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUhispania

Xabi Alonso akabiliwa na shinikizo kufuatia kipigo

11 Desemba 2025

Kocha wa Real Madrid Xabi Alonso ameonyesha msimamo wa kipekee wa uongozi baada ya kikosi chake kupoteza kwa mabao 2–1 mbele ya Manchester City katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa uliopigwa uwanjani Santiago Bernabéu.

Bundesliga | Bayer Leverkusen vs SV Werder Bremen
Kocha wa Real Madrid Xabi AlonsoPicha: Rolf Vennenbernd/dpa/picture alliance

Kocha wa Real Madrid Xabi Alonso amewashukuru wachezaji wake kwa kujituma uwanjani licha ya kipigo cha mabao 2-1 mbele ya Manchester City katika mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya iliyochezwa uwanjani Santiago.

Alonso amesema anaamini klabu hiyo itarejea kwenye kiwango chake cha kawaida hivi karibuni.

Miamba hao wa Uhispania wamepata ushindi katika mechi mbili pekee kati ya nane zilizopita katika mashindano yote.

Matokeo hayo yameongeza shinikizo kwa Alonso huku vyombo vya habari nchini humo vikiripoti juu ya kuwepo kwa mgawanyiko kati ya kocha huyo na baadhi ya wachezaji wake, ingawa wachezaji kadhaa wamejitokeza hadharani na kuonyesha kumuunga mkono.

Kwengineko, klabu inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, Bayer Leverkusen imetoka sare ya 2-2 na Newcastle United katika mchezo wa kusisimua wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Alejandro Grimaldo alifunga bao dakika ya 88 ya mchezo na kuhakikisha wanagawanya alama na Newcastle.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW