AMAGASAKI. Ajali ya gari moshi yaua watu 53 nchini Japan.
25 Aprili 2005Matangazo
Watu wasiopungua 53 wameuwawa na wengine zaidi ya 400 wakajeruhiwa katika ajali mbaya ya garimoshi la abiria kuwahi kutokea nchini Japan. Maafisa wanaamini dereva wa garimoshi hilo alikuwa akiliendesha kwa kasi na akashindwa kulidhibiti alipofika kwenye kona.
Mabehewa manne kati ya mabehewa saba ya garimoshi hilo yaliwacha reli na kuanguka huko Amagasaki, kilomita 400 magharibi mwa Tokyo.