1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waokozi wapo katika kuwanusuru watu 41 katika handaki India

23 Novemba 2023

Waokoaji nchini India wanaendelea kuchimbua sehemu iliyobaki ya vifusi ili kuwafikia wafanyakazi 41 walionasa kwa zaidi ya wiki mbili kwenye handaki la barabarani lililoporomoka.

Indien Uttarakhand Tunneleinsturz
Picha: AP Photo/picture alliance

Magari ya wagonjwa yanasubiri katika eneo hilo, yakijiandaa kuwasafirisha watu hao ambao maafisa wanatumai wataokolewa hivi karibuni kutoka kwenye handaki la jimbo la Himalaya la Uttarakhand. Wahandisi wamekuwa wakichimbua kwa siku kadhaa ili kupitisha bomba la chuma lenye urefu wa mita 57 katika mchanga, saruji na vifusi ambavyo vimewafungia ndani watu hao tangu sehemu ya handaki hilo linalojengwa ilipoporomoka Novemba 12. Juhudi za uokoaji zimetatizwa na vifusi vinavyoanguka pamoja na kuharibika mara kwa mara kwa mashine muhimu za kuchimba. Wafanyakazi hao walionekana wakiwa hai kwa mara ya kwanza Jumanne wiki hii, wakichungulia kwenye kamera iliyoingizwa ndani na waokoaji katika bomba jembamba ambalo wanalitumia kupata hewa safi, chakula, maji na umeme.