1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amenya asema maisha yako hatarini

1 Oktoba 2024

Mfichuzi wa sakata la mpango wa kampuni ya Adani ya India kutaka kuchukuwa imiliki wa uwanja mkuu wa ndege nchini Kenya, Nelson Amenya, amesema anakhofia uhai wake na kwamba maisha yake yako hatarini.

Kenya| Nairobi
Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta nchini Kenya.Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Amenya alisema alikubali kufichuwa mpango huo kwa sababu hivi sasa yuko nchini Ufaransa anakosoma, lakini anaweza kulengwa na mahasimu wake hata akiwa nje ya Kenya.

Ufichuzi wa Amenya ulichochea hasira nchini Kenya na kusababisha mgomo mkubwa uliofanywa na wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta pamoja na kuanzishwa uchunguzi kamili bungeni kuhusu mpango huo.

Soma zaidi: Bima ya afya ya umma yaanza Kenya

Wiki iliyopita, Waziri wa Fedha John Mbadi alikiri kwamba alishtushwa kugundua kwamba Mamlaka ya Usimamizi wa Uwanja wa Ndege ya Kenya (KAA)  ilichukua siku moja tu kuidhinisha pendekezo la kampuni ya Adani mnamo mwezi Machi 2024.