1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amir wa Qatar, mawaziri wa Ghuba waenda Iran kumzika Raisi

23 Mei 2024

Amir wa Qatar na mawaziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait wamekwenda Tehran kuhudhuria maziko ya Rais Ebrahim Rais.

Iran Teheran| Makamu wa Rais wa Iran Mohammad Mokhber
Kaimu Rais wa Iran Mohammad Mokhber akimakaribisha Sultana wa Oman Haitham bin Tariq kwenye msiba wa Rais Ebrahim Raisi.Picha: Majid Asgaripour/WANA/REUTERS

Amir wa Qatar na mawaziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait wamekwenda Tehran kuhudhuria maziko ya Rais Ebrahim Raisi, ambaye chini ya uongozi wake yamefikiwa makubaliano ya kihistoria yaliorekebisha uhusiano katika Tehran na majirani wa kanda ya Ghuba.

Rais na waziri wa mambo ya nje Hossein Amirabdollahian, pamoja na abiria wengine sita na wafanyakazi waliuawa katika ajali ya helikopta nchini Iran siku ya Jumapili.

Soma pia: Mamilioni ya waombolezaji wajitokeza kutoa heshima zao kwa Rais Ebrahim Raisi

Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani, aliongoza ujumbe uliohusisha waziri mkuu Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani, ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa Qatar.

Kituo cha televisheni cha Saudi Arabia cha Al Arabiya, kilisema waziri wa mambo ya nje wa Saudia Mwanamfalma Faisal bin Farahn atahudhuria maziko, huku vyombo vya habari vya Iran vikimuonyesha waziri wa mambo ya nje wa UAE Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan akiwa msibani na kutoa heshima kwa marehemu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW