1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMISOM yauwa wanamgambo 14 wa al-Shabaab

6 Juni 2017

Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kinasema kuwa askari wake wamewauwa wapiganaji 14 wa kundi la Al-Shabaab katika mapambano nchini Somalia.

African Union Soldaten in Somalia
Picha: AFP/Getty Images/A. Hashi Nor

Kwa mujibu wa ukurasa wa Twitter wa AMISOM, wanajeshi waliwagundua wapiganaji hao wakati wa doria katika mji wa kusini wa bandari wa Kismayo jana Jumatatu (5 Juni).

Miongoni mwa waliouawa ni pamoja na kamanda wa ngazi za kati wa Al-Shabaab.

AMISOM inaisadia serikali ya Somalia katika mapambano yake dhidi ya al-shabaab kupitia wanajeshi na maafisa wa polisi karibu 22,000.

Kundi hilo la kijeshi linalotaka kuunda taifa la Kiislamu nchini Somalia, lina mafungano na mtandao wa kigaidi wa kimataifa wa al-Qaida.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW