1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amman: Mwanaharakati wa mtandao wa al-Qaida auliwa huko Jordan.

9 Januari 2007

Maafisa wa usalama nchini Jordan wanasema mtu anayeshukiwa kuwa ni mpiganaji wa mtandao wa al-Qaida ameuwawa na mwengine amekamatwa katika mji wa kaskazini wa Irbid. Televisheni ya serekali ya Jordan iliripoti kwamba idadi kadhaa ya wanajeshi wa usalama walijeruhiwa katika operesheni hiyo. Mshukiwa aliyeuwawa anasemekana ana paspoti ya muda ya Jordan, hiyo inamaanisha yeye ni Mpalastina wa kutokea Ukanda wa Gaza. Polisi waliyavamia maficho katika mji wa Irbid wakiambiwa kwamba wapiganaji wa mtandao wa al-Qaida walikuwa wanafanya njama ya kufanya mashambulio katika Jordan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW