AMMAN:Waziri Steinmeier avunja ziara ya Syria
16 Agosti 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Frank –Walter Steinmeier amevunja ziara yake ya Syria.
Waziri Steinmeier amewaambia wandishi habari mjini Amman kuwa uamuzi wake umesababishwa na hotuba ya rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo ya kuwasifu wapiganaji wa Hezbollah.
Katika hotuba yake rais Assad amewapongeza wapiganaji hao kwa alichoita ushindi azizi dhidi ya Israel kusini mwa Lebanon. Bwana Assad amesema ni jambo la fahari kwa nchi yake kuwaunga mkono wapiganaji wa Hezbollah.