1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUganda

Amnesty: Uganda ishinikizwe kufuta sheria dhidi ya ushoga

22 Oktoba 2025

Shirika la Kimataifa la Amnesty limeitaka Benki ya Dunia kuishinikiza serikali ya Uganda kufuta sheria kali dhidi ya watu wanashiriki mapenzi ya jinsia moja kabla ya kurejeshwa tena kwa ufadhili uliokuwa umesitishwa.

Washington DC I Ofisi za Benki ya Dunia
Ofisi za Benki ya Dunia jijini Washington, MarekaniPicha: ullstein bild - Fotoagentur imo

Wito wa Amnesty umetolewa baada ya Afisa mmoja wa wizara ya fedha nchini Uganda kusema mapema wiki hii kwamba nchi hiyo itapokea kwa muda wa miaka mitatu jumla ya dola bilioni 2 kutoka kwa  Benki ya Dunia  ambayo ilisitisha mikopo yote kwa Uganda baada ya rais Yoweri Musevi kusaini mwaka 2023 sheria hiyo dhidi ya jamii ya LGBTQ+.

Wakati huo Benki ya Dunia ilisema kuwa miradi yote inayoifadhili inapaswa kuzingatia sera zake zisizo za kibaguzi. Sheria ya  Uganda dhidi ya ushoga ni mojawapo ya sheria kali zaidi duniani ikijumuisha wakati mwengine hukumu ya kifo katika baadhi ya matukio.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW