1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty: Haki za binadamu duniani zinakabiliwa na vitisho

24 Aprili 2024

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty limeripoti kuwa haki za binaadam zinazidi kukiukwa duniani kote na hali inazidi kuwa mbaya kwa miongo kadhaa sasa.

Amnesty International
Nembo ya Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty Picha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Katika ripoti yake kila mwaka iliyotolewa leo Jumatano shirika la Amnesty International  limeangazia migogoro ya Gaza na Ukraine pamoja na kuenea kwa serikali za kimabavu ambazo zinaharibu utaratibu wa kimataifa kwa kukiuka sheria za kimataifa na kutojali haki za kimsingi.

Katibu Mkuu wa shirika hilo Agnès Callamard amesema kuongezeka kwa migogoro ya silaha, Gaza, Ukraine na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Sudan, Ethiopia na Myanmar akihoji kuwa utaratibu wa kimataifa unaotegemea kanuni uko katika hatari ya kuangamizwa.

Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa lajadili kusitisha mauzo ya silaha kwa Israel

Miongoni mwa mambo mengine, ripoti hiyo inakosoa pia matumizi ya Marekani ya kura yake ya turufu 
kulemaza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa miezi kadhaa juu ya azimio la kusitisha mapigano Gaza.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW