1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Amnesty International lafunga virago India

29 Septemba 2020

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesimamisha shughuli zake nchini India, likisema serikali imezizuia akaunti zake za benki.

Indien Amnesty International
Picha: Aijaz Rahi/AP Photo/picture-alliance

Amnesty International limesema limewaachisha kazi wafanyakazi wake baada ya kuandamwa na serikali katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kuhusiana na madai ya kadhia inayohusishwa na makosa ya kifedha,madai ambayo shirika hilo linasema hayana msingi.

Katika taarifa yake shirika hilo la kimataifa la kutetea haki za binadamu limeeleza kwamba haya ni matukio ya karibuni kabisa ya serikali ya India kuyaandamana mashirika ya haki za binadamu kwa misingi ya madai ya kuchochewa na ambayo haya ukweli.

Maafisa wa shirika la Amnesty wakiwa na nakala za ripoti wakati wa kutangazwa kwake mjini Sirinagar, Kashmir ya India, Septemba 13, 2017.Picha: Mukhtar Khan/AP Photo/picture alliance

Ukiukaji wa haki za binadamu

Akaunti za benki ya shirika hilo ilizuiwa Septema 10 kwa mujibu wa maelezo yake. Na ikumbukwe kwamba katika miezi ya hivi karibuni shirika la Amnesty International liliwahi kuyaangazia matukio ya ukiukaji haki za binadamu katika maeneo yanayozozaniwa ya Jammu na Kashmir.

Soma pia: Amnesty imeilaumu Ulaya kwa mateso ya wahamiaji Libya

Shirika hilo pia liliripoti juu ya kile ilichokitaja kuwa ukosefu wa uwajibikaji wa polisi wakati wa maandamano ya mjini Delhi mnamo mwezi Februari,na kwahivyo kinachofanyika sasa ni kwamba serikali imeamua kulitia adamu shirika hilo.

Hata hivyo serikali ya India haijasema chochote hadi sasa. Wasemaji wa serikali waliotumiwa maombi ya kutoa tamko wote wamekaa kimya.

Wafanyakazi wa Amnesty Inernational wakiwa ofisini kwao katika makao makuu wa shirika hilo mjini Bangalore, India.Picha: Aijaz Rahi/AP Photo/picture-alliance

Serikali ya waziri mkuu Modi yalaumiwa

Serikali ya waziri mkuu Narendra Modi imekabiliwa na tuhuma kwamba inawaandama au kuwakandamiza wakosoaji ikiwemo watu wa Jimbo la Kashmirambalo wakaazi wake wengi ni waislamu na ambako wanamgambo wamekuwa wakipambana na vikosi vya serikali kwa zaidi ya miaka 30.

Soma pia: Amnesty International yamtaka rais Tshisekedi kutekeleza ahadi yake

Lakini pia wakosoaji wanasema serikali ya Modi inaitia msukumo agenda ya kuwatanguliza mbele Wahindu na kuhujumu misingi ya demokrasia ya kutoelemea dini nchini India na kuzusha hofu miongoni mwa jamii yake yawaislamuwaliowachache ambayo ni milioni 170.

Raia wauawa Jamhuri ya Afrika ya Kati

01:49

This browser does not support the video element.

Serikali ya India inakanusha kuwa na ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya jamii yoyote ile nchini humo.

Mwanasiasa wa upinzani Shashi Tharoor amesema hatua ya kujiondowa kwa shirika la Amnesty International nchini humo ni pigo kubwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW