1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty International lataka Jenerali Ndima achunguzwe, DRC

11 Desemba 2024

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linataka Luteni jenerali Constant Ndima wa DRC achunguzwe kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Gavana wa zamani wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Luteni jenerali Constant Ndima
Gavana wa zamani wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Luteni jenerali Constant NdimaPicha: Benjamin Kasembe/DW

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limetoa mwito wa kuchunguzwa gavana wa zamani wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Luteni jenerali Constant Ndima na maafisa wawili waandamizi jeshini, kuhusu kile huenda kilikuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Tuhuma hizo zinahusiana na hatua ya matumizi ya nguvu iliyochukuliwa kuzima  maandamano ya kuupinga ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo mwaka jana.

Shirika hilo la haki za binadamu limesema kwenye ripoti yake, kwamba kiasi watu 56 waliuwawa na 80 walijeruhiwa na vikosi vya usalama vya Kongo, wakati wa maandamano yaliyopangwa na kundi linalojiita Wazalendo yaliyofanyika katika mji wa Goma Agosti mwaka 2023.

Ripoti ya Amnesty International imesema Kanali Mike Kalamba Mikombe aliyekuwa akiongoza jeshi la ulinzi la kongo mjini Goma alituhumiwa kuamrisha wanajeshi wawafyetulie risasi waandamanaji waliokuwa hawana silaha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW