Amnesty International : Mamia wauwawa Iraq
28 Machi 2017Ripoti yao hiyo iliotolewa Jumatatu inafuatia kuungama kwa muungano huo kwamba jeshi la Marekani lilihusika na shambulio la anga la Machi 17 katika kitongoji kilioko magharibi ya mji wa Mosul ambapo wakaazi wamesema limeuwa zaidi ya raia mia moja.
Maafisa wa Marekani hawakuthibitisha kwamba kulikuwa na maafa ya raia lakini wameanzisha uchunguzi.Repoti hiyo ya Amnesty pia imetaja shambulio la pili lililiofanyika Jumamosi ambalo limeuwa takriban watu 150.Muungano unaongozwa na Marekani umesema katika taarifa kwamba inachunguza mashambulizi kadhaa magharibi ya Mosul ambayo inadaiwa yamesababisha vifo vya raia.
Milley amesema "Inawezekana kabisa kwamba kundi la Dola la Kiislamu imeliripuwa jengo hilo ili lawama ziwaungukie majeshi ya muugano na kusababisha kucheleweshwa kwa mashambulizi ya anga kwa mji wa Mosul na kwa hiyo hatujuwui bado ."
Nyumba zinangamizwa na familia zote
Ushahidi uliokusanywa na shirika hilo huko Mosul unaonyesha mwenendo wa kutisha wa mashambulizi ya anga ya muungano unaoongozwa na Marekani ambayo yameangamiza nyumba nzima zikiwa na familia zao zote.
Ripoti hiyo inasema kushindwa kuchukuwa tahadhari kuzuwiya vifo vya raia utakuwa ni ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa ya ubinaadamu.
Mjini Baghdad mkuu wa utumishi jeshini Generali Mark A. Milley ambaye yuko ziarani nchini Iraq amesema hapo Jumatatu kile kilichosababisha mripuko katika jengo lilioko katika eneo hilo bado hakijulikani.
Milley amesea "Inawezekana kabisa kwamba kundi la Dola la Kiislamu imeliripuwa jengo hilo ili lawama ziwaangukie majeshi ya muugano na kusababisha kucheleweshwa kwa mashambulizi ya anga kwa mji wa Mosul na kwa hiyo hatujuwui bado ."
Kuongezeka mashambulizi ya anga na mizinga
Milley amewaambia waandishi wa habari baada ya kukutana na maafisa wa wizara ya ulinzi ya Iraq kwamba sababu itajulikana siku zinazokuja baada ya uchunguzi.
Vikosi vya Iraq vilianza kuushambulia mji wa Mosul unaoshikiliwa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu hapo mwezi wa Oktoba baada ya maandalizi ya miezi kadhaa na mazoezi.Hapo mwezi wa Januari Iraq ilitangaza nusu ya Mosul ya mashariki yaani Mto Tigris wenye kuugawa mji huo kati ya mashariki na magharibi imekombolewa.Serikali ya Iraq hivi sasa inapambana kukombowa upande wa pili wa magharibi wa mji huo.
Mashirika ya kiraia na yale ya haki za binaadamu pamoja na maafisa wanaofuatilia mashambulizi hayo mara kwa mara yamekuwa yakionya juu ya uwezekano wa kuongezeka kwa vifo vya raia huko Mosul ya magharibi kutokana na mkusanyiko mkubwa wa watu katika eneo hilo na kuzidi kutegemewa kwa mashambulizi ya anga na mizinga kuukombowa mji huo.
Mwandishi : Mohamed Dahman/AP
Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman