1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty yalaani matumizi ya risasi za mpira kote ulimweguni

14 Machi 2023

Shirika la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limeonya kuhusu matumizi ya risasi za mpira zinazotumiwa na polisi dhidi ya maandamano ya amani.

Weltspiegel | Johannesburg, Südafrika | Unruhen nach Verhaftung von Jacob Zuma
Picha: Luca Sola/AFP

Shirika la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limeonya kuhusu matumizi ya risasi za mpira zinazotumiwa na polisi dhidi ya maandamano ya amani. Shirika hilo limesema matukio hayo yamezidi duniani na kupelekea majeraha mengi ya macho na hata vifo.

Baada ya kufanya utafiti kwa mataifa 30 ndani ya miaka mitano, shirika hilo lililo na makao yake makuu mjini London limetoa wito wa udhibiti wa kimataifa wa biashara na kutoa wito wa matumizi madogo ya silaha za mauaji.

Katika ripoti yake mpya iliyoipa jina la  "Jicho langu limeripuka" imesema maelfu ya waandamanaji na watu wasiohusika na maandamano wamejeruhiwa na kuuwawa kufuatia polisi kutumia nguvu kupitia kiasi dhidi ya waandamanaji.

Miongoni mwa silaha zilizotajwa ni risasi za mpira, mabomu ya kutoa machozi, makombora yaliyorushwa moja kwa moja kwa waandamanaji katika maeneo ya Kusini na Amerika ya Kati, Ulaya, Mashariki ya Kati, Afrika na Marekani.