1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty: Kongo ilinde haki za wakaazi maeneo ya viwanda

4 Juni 2024

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty, limesema mamlaka ya Jamhuri ya Kongo haijachukuwa hatua za kutosha kuhakikisha viwanda vinalinda haki za binadamu na mazingira katika jamii ambazo watu wanaishi.

DR Kongo | Haki za Binadamu | Mkuu wa Amnesty Internationa Agnes Callamard
Mkuu wa shirika la Kutetea Haki za Binadamu Kimataifa Amnesty Agnes Callamard, wakati wa uwasilishaji ripotiPicha: Michel Euler/AP/picture alliance

Amnesty International imetoa kauli hiyo baada ya kuangazia hali ya kuvuja kwa mafuta na moshi unaotokana na shughuli zinazofungamanishwa  na kampuni za mafuta za TotalEnergies EP Kongo, Wing Wah na Metssa Kongo, pamoja na athari zake katika maeneo ya Pointe-Noire (POEINT NUARR)  na Kouilou (KWILUU) ambayo yako kwenye pwani ya Atlantiki.

Ripoti iliyotolewa na Amnesty, imeonesha kuwa mbali na utajiri unaotokana na shughuli za  viwanda nchini Kongo, wanavijiji wanakabiliwa na ukiukwaji wa haki za kimazingira, kiuchumi na kijamii.

Samira Daoud, mkurugenzi wa shirika hilo la Amnesty International katika kanda ya Afrika Magharibi na Kati, amesema shirika hilo linatoa wito kwa mamlaka kuhakikisha biashara zinafanya kazi kwa kuwajibika na kuzingatia majukumu yao ya mazingira na haki za binadamu.

Soma pia:Amnesty yaitaka Kongo ichukue hatua za kulinda haki za raia

Amnesty imesema baada ya kuwasilisha ripoti yake kwa kampuni hizo, TotalEnergies EP Kongo na Metssa Kongo zilijibu maswali yaliokuwemo. 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa TotalEnergies EP Kongo, tawi la kampuni ya mafuta ya Ufaransa TotalEnergies, iliandikisha angalau umwagikaji wa mafuta mara tatu kutoka mwaka 1972 hadi 2011 ambayo yalisababisha mafuta ghafi kuvuja kwenye ziwa dogo lililo karibu.

Kampuni hiyo lakini inadaiwa kuchukua hatua ya kusafisha umwagikaji huo wa mafuta.  
Amnesty pia imesema hakuna uchafuzi wowote ulioripotiwa kufanywa kwenye maji, baada ya uchunguzi uliofanywa mwaka 2021.   

Amnesty: Kuna madhara miongoni mwa wakaazi

Shirika hilo la haki limeongeza kwamba wakazi wengi walilalamikia ukosefu wa taarifa, na kuripoti kuhusu matatizo ya afya, hasa kuhara, baada ya kula samaki kutoka kwenye ziwa hilo dogo.

Wavuvi wakiwa kando ya mtoPicha: JOHN WESSELS/AFP

Kulingana na Amnesty, kampuni hiyo haikuwahi kutangaza hadharani matokeo ya uchunguzi  huo wa maji wa 2021 na kuongeza kuwa mamlaka haijawahi kuchunguza uwezekano wa madhara ambayo mafuta huenda yalisababisha.

Amnesty pia imesema mamlaka nchini humo pamoja na kampuni hizo hazitoi taarifa kamili hadharani baada ya matukio hayo ya kimazingira.

Soma pia:Kundi la kutetea haki za binadamu lataka uchunguzi kuhusu 'mauaji' ya baada ya mapinduzi, Kongo

Ripoti hiyo ya Amnesty imesema lazima serikali iweke hadharani matokeo ya uchunguzi wa  mazingira unaofanywa baada ya tukio lolote na kwamba kampuni zote zinahitaji kurekebisha kikamilifu uharibifu wa mazingira unaohusishwa na shughuli zao na kulipa fidia kwa waathirika kulingana na sheria ya Kongo.

Kuchafuliwa kwa vyanzo va maji 

Mto Kongo wafurika, wakazi wahangaishwa na mafuriko

02:29

This browser does not support the video element.

Kulingana na Amnesty, wakaazi walishutumu kampuni ya petroli na gesi ya China ya Wing Wah kwa kuchafua mto Loeme, huku kukiwa na uwazi mdogo kuhusu hatua za kufuatilia baada ya kumwagika kwa mafuta.

Ripoti hiyo pia imesema huko Vindoulou, kitongoji kilicho nje kidogo ya Pointe-Noire, kundi la wakaazi limelalamika kwa miaka mingi kuhusu moshi kutoka kwa kiwanda cha kuchakata cha Metssa Kongo kilicho umbali wa mita 50 tu kutoka shule moja.

Kampuni hiyo ambayo ni tawi la kundi la makampuni la India, Metssa hutengeneza vipande  vya madini ya risasi na sampuli kutoka kwa watu wanaoishi karibu na kiwanda hicho zilizochukuliwa mwaka wa 2023 zilifichuwa viwango vya juu vya madini hiyo ambavyo kulingana na viwango vya Shirika la Afya Ulimwenguni, sio salama.

Soma pia:Kongo yaishutumu Apple kwa matumizi ya ''madini ya damu''

Mettsa Kongo, inasema ilipata leseni kutoka eneo hilo mnamo mwaka 2018 na cheti cha ubora mwaka jana.

Amnesty inasema mamlaka ya Kongo na Wing Wah hazikujibu maswali kutoka shirka hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW