1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Amnesty laishutumu Iran kwa kuwanyonga watu 173

2 Juni 2023

Amnesty International limesema hatua hiyo imeonesha ukosefu wa ubinadamu nchini Iran.

Kanada Toronto Protest gegen Hinrichtungen im Iran
Picha: Mert Alper Dervis/AA/picture alliance

Mamlaka nchini Iran zimetekeleza adhabu ya kuwanyonga kiasi watu 173 mwaka huu, walioshtakiwa kwa makosa yanayohusiana na usafirishaji madawa ya kulevya.

Hayo yameelezwa leo na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International,ambalo limesema idadi hiyo ni takriban mara tatu zaidi ya iliyoonekana mwaka jana.

Amnesty International limesema hatua hiyo imeonesha ukosefu wa ubinadamu nchini Iran na  kupuuzwa kwa haki ya mtu kuishi lakini pia ni hatua iliyokiuka sheria ya kimataifa.

Ripoti ya Amnesty International imeonesha kwamba idadi jumla ya watu walionyongwa kutokana na uhalifu kwa ujumla nchini Iran iliongezeka kwa kiasi kikubwa huku kiasi watu 282 wakinyongwa mwaka huu kwa ujumla.