1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Amnesty: Mali ichunguze shambulizi la droni dhidi ya raia

6 Novemba 2024

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limeutaka utawala wa kijeshi nchini Mali kuchunguza mauaji ya raia wanane, katika mashambulizi ya droni kaskazini mwa nchi hiyo.

Wanajeshi wa Mali na waasi wa zamani wa Tuareg wakishika doria ya pamoja mnamo Februari 23, 2017
Wanajeshi wa Mali na waasi wa zamani wa Tuareg wakishika doria ya pamoja Picha: Baba Ahmed/AP/dpa/picture alliance

Katika taarifa, Amnesty imesema mashahidi waliripoti kuwa takriban raia wanane, wakiwemo watoto sita, waliuawa katika mashambulizi ya anga kwenye soko lenye shughuli nyingi katika kijiji cha Inadiatafane, katika eneo la Timbuktu, mnamo Oktoba 21.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa watu wengine 15 walijeruhiwa, huku wengine wakiwa katika hali mahututi.

Shambulizi la droni lapaswa kuchunguzwa kama uhalifu wa kivita

Shirika hilo la kutetea haki pia limesema kuwa shambulizi hilo linapaswa kuchunguzwa kama uhalifu wa kivita kwasababu lilisababisha vifo na majeraha miongoni mwa raia huku miundo mbinu ya kiraia pia ikilengwa.

Utawala wa kijeshi Mali wajadili mikakati ya kudhibiti hali ya usalama

Hata hivyo serikali ya Mali haikujibu ombi la tamko kutoka kwa shirika la habari la Ufaransa AFP.

Serikali ya Mali inajitetea dhidi ya shutuma za mara kwa mara za makosa yanayodhuru raia.