1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty: Uganda inawakandamiza wapinzani kabla ya uchaguzi

5 Januari 2026

Shirika la kimataifa la haki za binaadamu la Amnesty International limesema hii leo kwamba vikosi vya usalama vya Uganda vimekuwa vikiwatesa na kuwakamata kiholela wapinzani kwa lengo la kuwatisha

Uganda 2026 | Rais Yoweri Museveni amewaonya waandamanaji wakati wa uchaguzi
Rais Yoweri Museveni awaonya waandamanaji kabla ya uchaguzi wa 2026, akisema polisi wamejipanga vyema kukabiliana na machafuko. Alijibu maoni ya mpinzani mkuu Robert Kyagulanyi Ssentamu kuhusu waandamanaji kuwa wengi kuliko polisi.Picha: Presidential Press Unit, PPU

Uganda inatarajiwa kufanya uchaguzi Januari 15.

Shirika hilo limekusanya vithibitisho vya maafisa wa usalama kuwapiga na kutumia gesi ya kutoa machozi dhidi ya wafuasi wa chama cha upinzani cha National Unity Platform NUP kinachoongozwa na Bobi Wine.

Mkurugenzi wa Amnesty wa kanda ya mashariki na kusini mwa Afrika Tigere Chagutah amesema, serikali imeanzisha kampeni ya kikatili ya kuwakandamiza wapinzani na wafuasi wao hali inayowawekea mazingira magumu ya kufanya mikusanyiko ya amani.

Aidha, upo wasiwasi kwamba huenda serikali ikazima intaneti wakati wa uchaguzi, kama ilivyofanya mwaka 2021 ili kuzuia usambazaji wa taarifa kuhusiana na udanganyifu wa kura na machafuko.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW