Amnesty yaituhumu Mali kutochunguza uhalifu wa kivita
13 Aprili 2022Matangazo
Shirika hilo limehoji kuwa uvunjifu wa sheria kiholela unaendelea kutokana na visa kama hivyo.
Kwenye ripoti yake, Amnesty International imesema visa vya machafuko na uhalifu wa kivita dhidi ya raia vimeongezeka tangu mwaka 2018 hususan nchini Mali, taifa linalozongwa na machafuko.
Shirika hilo limeainisha visa kadhaa vya mauaji ya watu wengi yanayodaiwa yalifanywa na wanamgambo wenye itikadi kali za kidini, vikosi vya Mali na vilevile jeshi la Ufaransa ambalo lilikuwa la kwanza kuingia nchini humo mwaka 2013 kupambana na wanamgambo.