Amnesty yakosoa hatua za Trump akitimiza siku 100 madarakani
29 Aprili 2025
Matangazo
Amnesty imesema hatua za Trump zinalenga kurejesha nyuma mafanikio yaliyopatikana katika vita dhidi ya umaskini duniani, kupambana na ubaguzi wa rangi na vipaumbele muhimu vya haki za binadamu.
Tangu alipoapishwa kuongoza muhula wa pili mnamo Januari 20, Trump amechukua hatua kadhaa ambazo zimeutikisa ulimwengu kiuchumi, kijamii na kiusalama.
Baadhi, ni hatua za ushuru, kusitisha misaada ya kimataifa, sintofahamu na washirika wake wa NATO pamoja na vitisho vya kunyakuwa maeneo kama Gaza, Greenland, Mfereji wa Panama na kutaka kuifanya Canada kuwa jimbo la 51 la Marekani.