1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty yaonya Kombe la Dunia kuwa 'jukwaa la ukandamizaji'

30 Machi 2026

Ripoti mpya ya shirika la haki za binaadamu iliyotolewa leo imeonya kwamba mashindano ya Kombe la Dunia mwaka huu yanaweza kugeuka kuwa jukwaa la ukandamizaji na matendo ya kidikteta.

Kombe la Dunia 2026 | Uswisi vs. Ujerumani | mechi ya kirafiki
Mechi ya kirafiki kuelekea michuano ya Kombe la Dunia 2026 kati ya Ujerumani na Uswisi iliyochezwa tarehe 27 Machi 2026.Picha: Heiko Becker/HMB Media/picture alliance

Ripoti ya shirika hilo yenye kurasa 36 iliyopewa jina "Ubinaadamu Lazima Ushinde: Kulinda haki, kukabiliana na ukandamizaji kwenye Kombe la Dunia la FIFA 2026" inachambuwa kwa kina matukio yanayoweza kuhatarisha haki za mashabiki, wachezaji, waandishi wa habari, wafanyakazi na jamii za wenyeji kwenye mataifa hayo matatu.

Ikiwa ni miezi michache kuelekea michuano hiyo, Marekani bado imeweka marufuku ya kuingia nchini humo kwa baadhi ya nchi ambazo zimefaulu kushiriki kombe hilo litakalokuwa na mechi 48.

Michuano hiyo inayotazamiwa kuhudhuriwa na mamilioni ya mashabiki wa soka inaanza mnamo Juni Mosi kwa maechi kati ya Meksiko na Afrika Kusini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW