1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan: Amri ya kusitisha vita kwa muda wa saa 24 yaanza.

10 Juni 2023

Makubaliano ya kusitisha vita kwa muda wa saa 24 yameanza leo Jumamosi kati ya majenerali wanaozozana nchini Sudan lakini hofu imetanda ya kusambaratika makubaliano hayo sawa na yaliotangulia.

Sudan | Unruhe in Khartoum
Picha: AP

Wapatanishi wa mazungumzo ya amani kati ya pande hizo mbili Marekani na Saudi Arabia zimeonya kwamba huenda zikasitisha juhudi za upatanishi.

Makubaliano hayo yaliotangazwa na Marekani na Saudi Arabia siku ya Ijumaa yameanza kutekelezwa leo Jumamosi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi.

Wapatanishi hao wamesema kuwa iwapo pande hizo mbili zitashindwa kuzingatia makubaliano hayo ya kusitisha mapigano kwa saa 24, itawalazimu kufikiria kuahirisha mazungumzo katika mji wa Jeddah nchini Saudi Arabia ambayo yamesitishwa tangu mwishoni mwa mwezi uliopita.

Raia wamekatishwa tamaa kwamba usitishaji huo wa mapigano uliokuwa umeahidiwa ni wa muda mfupi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW