Amri ya kutotoka nje yawekwa BurkinaFaso kupambana na ugaidi
5 Machi 2023Matangazo
Uasi wa muda mrefu katika taifa hilo la Sahel umesbabisha mauaji ya maelfu ya watu, polisi na wanajeshi huku zaidi ya watu milioni mbili wakikimbia makaazi yao.
Taarifa ya Katibu Mkuu ya serikali ya jimbo la Kaskazini, Kouilga Albert Zongo imesema chini ya mpango wa kupambana na ugaidi amro ya kutotoka nje usiku itaanza kutekelezwa kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi na moja alfajiri kuanzia tarehe 3 hadi tarehe 31 mwezi Machi.
Amri hiyo pia imepiga marufuku magari na pikipiki kuwepo barabarani ndani ya muda huo uliotolewa. Zongo amesema amri hiyo itaisadia jeshi kupambana na ugaidi katika eneo hilo linalopakana na Mali kulikoanzia uasi mwaka 2015.