1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amsterdam: Mtuhumiwa wa kumuuwa Van Gogh akiri amefanya hivyo

12 Julai 2005

Huko Uholanzi mtu anayeshukiwa katika kesi ya kuuliwa, mtengenezaji filamu maarufu, marehemu Van Gogh, amekiri kufanya hivyo. Hapo kabla, muendeshaji mashtaka alitaka mtuhumiwa, raia wa Kiholanzi mwenye asili ya Moroko, apewe kifungo cha maisha gerezani. Alihoji kwamba mauaji hayo yalifanywa kwa madhumuni ya kigaidi na yalikusudia kuichafua jamii ya Uholanzi. Upande wa mashtaka ulisema Mohamed Bouyeri, mwenye umri wa miaka 27, ambaye alizaliwa na kukulia Amsterdam, ni Muislamu mwenye siasa kali. Katika tamko la mwisho, muendeshaji mshtaka wa Uholanzi, Fritz van Straelen, alisema lengo la mshtakiwa lilikuwa kusababisha hofu miongoni mwa wakaazi wa Uholanzi na kuichafua kabisa misingi ya kisiasa, kiuchumi na ya kijamii ya Uholanzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW