1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMSTERDAM : Ndege ya Marekani yasindikizwa na ndege za vita

24 Agosti 2006

Ndege za kivita za Uholanzi zimeisindikiza ndege ya shirika la ndege la Marekani Northwest iliokuwa ikielekea India kurudi katika uwanja wa ndege wa Schifol mjini Amsterdam hapo jana baada ya wafanyakazi wa ndege kuripoti kuwepo kwa abiria waliozusha mashaka kwa vitendo vyao.

Maafisa wa uwanja wa ndege wa Uholanzi wamesema rubani ya ndege hiyo aliamuwa kuirudisha ndege hiyo mara tu baada ya kuingia katika anga ya Ujerumani.Jumla ya abiria 12 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo iliokuwa ikielekea Mumbai walikamatwa na polisi wakati ndege hiyo ilipotuwa tena katika uwanja wa ndege wa Amsterdam.

Polisi ya Uholanzi haikutaja uraia wa watu hao na kile kilichosababisha mashaka dhidi yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW