1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwandishi Habari wa Mexico ashinda tuzo ya DW

19 Februari 2019

Deutsche Welle imemtunuku tuzo ya uhuru wa kujieleza ya mwaka 2019 mwandishi wa habari za uchunguzi kutoka Mexico, Anabel Hernandez kwa ujasiri wake wa kufichua maovu ikiwemo rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Anabel Hernández
Picha: Imago

Anabel Hernandez ambaye ni mzaliwa wa Mexico, alianza kazi yake ya Uandishi wa habari mwaka 1993 wakati akiwa mwanafunzi huku akifanya kazi katika gazeti la kila siku la Reforma. Miaka iliyofuata Hernandez alijijengea jina lake kama mwandishi mkubwa wa habari za uchunguzi nchini Mexico.

Aliandika makala mbalimbali juu ya rushwa serikalini, unyanyasaji wa kingono na biashara ya madawa ya kulevya.

Aliweka wazi ukweli wa kushangaza katika vitabu vyake viwili juu ya maofisa wa serikali na wanaojihusisha na wauzaji wa madawa ya kulevya. Swala hilo lilikua na athari mbaya kwake. Kwasasa Hernandez anaishi uhamishoni barani Ulaya.

Alipata vitisho vya kuuliwa yeye pamoja na kwa watoto wake, kwahiyo ilibidi aikimbie Mexico.

Kazi yake ya kwanza ya uchunguzi ilitokea mwaka 2001. Iliangalia maisha ya kifahari katika kipindi cha urais wa Vicente Fox. Alitunukiwa tuzo ya National Journalism Prize (uandishi wa habari wa taifa) nchini Mexico kwa sababu ya kazi hiyo.

Ingawa baadaye gazeti la Milenio alilokua akilifanyia kazi lilizuia kazi zake zingine, kama njia ya kujiepusha na kufanyiwa fujo na kujiingiza kwenye migogoro.

Uthabiti dhidi ya vitisho vya wauza dawa za kulevya

Picha: DW/V. Tellmann

Hernandez aliandika kitabu kilichoitwa Narcoland kuhusu dawa za kulevya na wale waliokuwa wa wakiitetea.

Kitabu hicho kilifichua kuhusu wahusika wa biashara za madawa ya kulevya na pia kilionyesha jinsi yanavyohusishwa na maisha ya kila siku ya wamexiko. Kilionyesha pia siri za wanasiasa, wanajeshi na wafanyabiashara pamoja na wauzaji wa madawa ya kulevya.

Kitabu hicho kiliuzwa sana na kupelekea Hernandez kutishiwa kuuliwa. Kati ya hivyo vitisho, vilikua ni kuwekewa maiti za wanyama waliokua wamechinjwa mbele ya mlango wako, kama alivyolieleza jarida la national magazine mwaka 2013.

Kuanzia hapo akawa anatembea na walinzi kila sehemu. Ukweli unaosikitisha ni kwamba waliokua wanamtishia kumuuwa walikua sio wale wanaojihusisha na madawa ya kulevya bali watu waliotoka serikalini na ofisa wa juu kabisa kutoka jeshi la Polisi la Mexico, anaelezea mwandishi huyo wa habari.

Kisa cha watoto 43 na kitabu cha Hernandez

Picha: Verso Books

Wakati watoto 43 walipopotea nchini Mexico alitumia vyanzo vyake vya habari kuchunguza tukio hila na kupelekea kuandika kitabu juu ya Mauaji nchini Mexico na Hadithi ya Ukweli kuhusu watoto 43 waliopotea.

Hernandezi aliunganisha shuhuda mbalimbali na kuzilinganisha na ripoti maalum kutoka vyombo husika na kuandika nini kilichotokea usiku ule watoto hao walipopotea.

Kitabu hicho kinaonyesha jinsi maofisa wa serikali, pamoja na wanajeshi huku wakiungwa mkono na makundi ya wauza madawa ya kulevya walivyoshiriki katika tukio hilo la kuuliwa wanafunzi hao.

Kutokana na kutokata tamaa kwake na jinsi alivyotia jitihada katika kazi yake ya uandishi wa habari za uchunguzi kupiga vita rushwa na kutumiwa vibaya madaraka nchini Mexico, Kujumlisha hali ya hatari anayopitia, Deutsche Welle imemtunukia tuzo ya uhuru wa kujieleza ya mwaka 2019.

Mwandishi: Harrison Mwilima/ DW Spanish

Mhariri: Hamidou Oumilkheir

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW