1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Anasa ya Kuazima – Hatari ya Kuchukua Mkopo

6 Agosti 2013

Tatizo linaanzia na ari ya kutaka kumiliki baiskeli mpya ya kifahari. JD hana fedha za kutosha lakini anashindwa kuvumilia na kuchukua mkopo – ingawa hajui atakavyoulipa mkopo huo. Je, somo hili litamuathiri vipi JD?

Mtoto anaendesha baiskeli
Picha: LAIF

Katika mchezo huu wa Noa Bongo Jenga Maisha yako tunakutana na Gideon ‘Giddy’ Leboo, afisa wa masuala ya mikopo kwenye benki. Giddy anafahamu vyema athari zinazotokana na mikopo, kwani yeye na rafiki zake wanakumbuka wakati mgumu waliopitia katika suala la usimamizi wa fedha zao. Na hapo Giddy anatueleza safari ya ujana wake.

Wakati rafiki mkubwa wa Giddy, JD anapowasili na baiskeli mpya shuleni, hakuna anayefahamu kwamba ameichukua kwa mkopo, na mkopo huo utahitaji kulipwa. Lakini ni wapi JD atatoa pesa kulipa mkopo huo? Yeye na rafiki zake, Giddy na Jenny, wanakubaliana kumtembelea muuzaji wa pesa ili kumwezesha JD kulipa deni lake. Lakini wanafahamu kwamba muuzaji huyo wa pesa si mjinga walivyomdhania. Marafiki hao watatu wana hata mawazo ya kijinga zaidi, wanatumbukia kwenye matatizo makubwa.

Mara nyingi watu hudhania mikopo ni njia ya mkato katika kutatua matatizo ya kifedha au kukuwezesha kununua vitu unavyotamani maishani, mfano simu ya mkononi au baiskeli. Lakini kukopa kunaweza kuwa karaha kama mtu hajapanga jinsi ya kuulipa mkopo. Watu wengi hasa vijana wanaweza kuingia mashakani kwa sababu hawapati pesa za kutosha kila mwezi kuweza kulipa mikopo wanayochukua.

Lakini Giddy amepata funzo na sasa anajaribu kuwaelimisha wasikilizaji wa mchezo huu wa redio. Ujumbe wake ukiwa, ni vizuri kuchukua mikopo kujistawisha, lakini wakati pesa hizo zinapotumiwa vibaya basi humuacha mtu mashakani maisha yake yote.

Noa Bongo Jenga Maisha Yako ni vipindi vinavyotayarishwa na Deutsche Welle na vinasikika katika lugha sita ikiwa ni pamoja na Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamhara.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi

Onesha taarifa zaidi