1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

ANC yashindwa katika kesi dhidi ya chama cha Zuma

26 Machi 2024

Mahakama moja ya Afrika Kusini Jumanne imeitupilia mbali kesi ya chama tawala nchini humo iliyokuwa inataka chama kimoja pinzani kifutiliwe mbali na kipigwe marufuku ya kushiriki uchaguzi unaokuja.

Rais wa AfrikaKusini Cyril Ramaphosa
Rais wa AfrikaKusini Cyril RamaphosaPicha: Denis Farrell/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Mahakama hiyo ya uchaguzi imesema upinzani wa chama cha African National Congress ANC kwa jinsi Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo ilivyoshughulikia kusajiliwa kwa chama cha uMkhonzo weSizwe haukuwa na mashiko na kuongeza kwamba, cham hicho kilistahili kuwasiliana na tume ya uchaguzi kwanza kabla kuwasilisha kesi mahakamani.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliyeiongoza nchi hiyo kati ya mwaka 2009 na 2018, aliyeondolewa madarakani kufuatia madai chungunzima ya ufisadi yaliyomkabili, alikiasi chama cha ANC na kuunda chama chake cha uMkhonto weSizwe au MK.

Umaarufu wake hasa katika mkoa wake wa nyumbani wa KwaZulu-Natal, unaotarajiwa kuwa eneo muhimu katika uchaguzi wa mwaka huu, umekisaidia chama cha MK kuibuka kama mojawapo ya vyama vinavyopigiwa upatu kupata kura nyingi katika uchaguzi huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW