1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ancelotti: Wachezaji wangu wanaathirika na msururu wa mechi

24 Aprili 2023

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema vijana wake wamedhamiria kucheza vyema katika hatua ya mwisho ya msimu baada ya kutoa ushindi wa 2-0 dhidi ya Celta Vigo hapo Jumamosi.

UEFA Champions League Finale | Liverpool FC vs Real Madrid
Picha: Adam Davy/PA Wire/dpa/picture alliance

Madrid ambao kwa sasa wanaishikilia nafasi ya pili katika msimamo wa La Liga pointi kumi na moja nyuma ya Barcelona ambao waliwalaza Atletico Madrid 1-0 Jumapili kwa bao la Ferran Torres, wamepangiwa kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya miamba wa England Manchester City.

Na Ancelotti anasema wachezaji wake wanaathirika na msururu wa mechi chungunzima.

"Si rahisi unapowasili saa kumi na mbili asubuhi Alhamis kutoka kwenye mechi na Jumamosi upo uwanjani tena, kwasababu hiyo nastahili kuangalia iwapo wachezaji wako sawa. Katika mechi mbili zilizopita katika La Ligadhidi ya Cadiz na leo, timu ilikuwa sawa kisaokolojia," alisema Ancelotti.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW