1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Andrich asaini mkataba mpya wa kusalia Leverkusen hadi 2028

16 Agosti 2024

Mkurugenzi wa michezo wa Leverkusen Simon Rolfes alimwita Andrich "nguzo kuu" ya klabu huku akisifia "uchezaji wake bora kwenye jukwaa la kimataifa".

Andrich
Kiungo wa kati wa Ujerumani na Leverkusen Andrich amesaini mkataba mpya wa kusalia BayArena hadi 2028Picha: Kai Pfaffenbach/REUTERS

Kiungo wa kati wa Ujerumani Andrich ameongeza mkataba wa kuitumikia Leverkusen hadi 2028.

Kiungo huyo ameichezea timu ya taifa ya Ujerumani kwa mara ya kwanza mwezi Novemba mwaka jana na tangu wakati huo ameichezea timu ya taifa michezo 10, na kujumuishwa kwenye kila mechi ya timu hiyo katika michuano ya Euro 2024.

Msimu uliopita, Leverkusen ilikuwa timu ya kwanza katika historia ya Bundesliga kucheza mechi zote za msimu bila kushindwa, na kushinda taji lao la kwanza la ligi ya Bundesliga.

Andrich bado yapo sana ndani ya uzi wa LeverkusenPicha: Ciro De Luca/REUTERS

Soma zaidi. Bayer Leverkusen kukipoiga na Stuttgart DFL-SUPER CUP

Katika taarifa, Andrich alisema Leverkusen ilikuwa ni "anwani sahihi kabisa.
 
"Ninapitia kipindi cha mafanikio zaidi cha maisha yangu na ninahisi njaa ya timu bado ni kubwa hata baada ya msimu huu maalum."

Mkurugenzi wa michezo wa Leverkusen Simon Rolfes alimwita Andrich "nguzo kuu" ya klabu huku akisifia "uchezaji wake bora kwenye jukwaa la kimataifa".

Leverkusen watafungua msimu wao katika Kombe la Super Cup la Ujerumani Jumamosi hii, wakiwakaribisha Stuttgart.