Andy Burnham awa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza
20 Julai 2026
Burnham anaingia ofisini na kuahidi kuutekeleza kile alichoita "mpango wa miaka 10" kwa ajili ya kushughulikia baadhi ya masuala ya msingi yanayoirudisha nyuma Uingereza.
Katika hotuba yake ya kwanza aliyoitoa katika ofisi yake iliyoko mtaa wa Downing, Burnham ameahidi kuwashawishi wapiga kura aliosema wamechoshwa na siasa, kuuonyesha ulimwengu kwamba Uingereza inaweza tena kuwa mahali penye utulivu.
Ameongeza "Uingereza inahitaji kuonyesha ulimwengu kwamba tunaweza kurejesha utulivu tena, na hiyo ndiyo changamoto yetu katika kuifanya siasa iwe ya manufaa. Ninajua watu hapa nyumbani wamechoshwa na siasa. Nawasikia na mimi nataka kuwa mkweli kwenu, hatujawa wazuri vya kutosha na tunahitaji kuwa bora zaidi. Tutakuwa wazuri zaidi."
Viongozi mbalimbali wamempongeza Andy Burham wakiwemo Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa pamoja na waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese, ambao kwa pamoja wameahidi kushirikiana naye.