1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Angela Merkel achaguliwa tena kuwa kansela wa Ujerumani

Oumilkheir Hamidou
14 Machi 2018

Siku 171 baada ya uchaguzi mkuu, bunge la Ujerumani Bundwestag limepiga kura hii leo kumchagua Angela Merkel kuwa kansela kwa mhula wa nne mfululizo.

Deutschland Bundestag Kanzlerwahl
Picha: Getty Images/AFP/O. Andersen

Zoezi la kumchagua kansela limeshakamilika katika bunge la shirikisho Bundestag. Lakini kama ilivyokuwa miaka minne iliyopita, na safari hii pia Angela Merkel hakupata kura zote za wabunge wa vyama vinavyounda serikali ya muungano. Wabunge 364, kati ya 399 wa vyama hivyo ndio waliomuunga mkono mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 63, ikimaanisha 35 kati ya wabunge wa kambi yake hawakumuunga mkono. Wabunge 315 wamempinga na tisa wamejizuwia kupiga kura.  Wabunge 702 kati ya 709 wa shirikisho ndio waliohudhuria kikao cha leo na kura za wabunge 692 zimehesabiwa kuwa halali.

Baada ya kuchaguliwa Angela Merkel alimjibu spika wa bunge Wolfgang Schauble na kusema

anayakubali matokeo ya uchaguzi."

Angela Merkel baada ya kuchaguliwa kuwa kansela kwa mhula wa nne hii leoPicha: Getty Images/AFP/J. MacDougall

Wolfgang Schäuble ambushuria uwezo, ufaniisi na baraka za Mungu

Baada ya kuchaguliwa kwa wingi wa vyama tawala, Angela Merkel ameelekea katika kasri la rais ambako rais wa shirikisho Frank-Walter Steinmeier alimkabidhi hati ya kuchaguliwa kwake kabla ya kurejea tena bungeni kuidhinishwa na spika wa bunge hilo Wolfgang Schäuble.

Mwanzoni mwa mhula wake wa tatu, miaka minne iliyopita, Angela Merkel alipungukiwa na kura 42 kutoka wabunge wa vyama tawala vya CDU/CSU na SPD. Na hata mihula miwili ya awali, mwaka 2005 na 2009 sio wabunge wote wa vyama tawala waliomuunga mkono.

 Naibu mwenyekiti wa chama cha uipinzani cha FDP Wolfgang Kubicki amesema matokeo ya uchaguzi wa kansela yanaashiria muungano sio wa vyama vikuu, bali  ni wa vyama vidogo. Anaashiria kuna wabunge wa SPD sawa na wa CDU ambao hawakumuunga mkono kansela. Anasema uamuzi wao hauashirii mema kwa serikali ya muungano.

Kikao cha kwanza cha baraza jipya la mawaziri kuitishwa leo jioni

Ofisi ya kansela mjini BerlinPicha: picture-alliance/W. Minich

Kwakua zoezi la uchaguzi katika bunge la shirikisho ni la siri, hakuna anaeweza kusemam kwa uhakika wangapi muiongoni mwa wabunge wa vyama tawala hawakumpigia kura au wangapi kutoka vyama vya upinzani wamempigia kura Angela Merkel.

Kama ilivyotajwa katika sheria msingi ya Ujerumani, magari ya fakhari yatakuwa yakenda na kurudi kati ya bunge la Reichtag na Schloss Bellevue , umbali wa kilomita mbili , kwenda kupokea hati za kuchaguliwa kwao, tangu kansela mpaka mawaziri wa serikali yake na kurejea baadae bungeni kuidhinishwa.

KIkao cha kwanza cha baraza jipya la mawaziri kitaitishwa leo jioni.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/dpa/

Mhariri: Iddi Ssessanga

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW