1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Angela Merkel ziarani Marekani

1 Mei 2014

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel leo anaanza ziara nchini Marekani ambako atakutana na rais wa nchi hiyo, Barack Obama. Agenda ya mazungumzo yao itajikita zaidi katika mzozo wa Ukraine unaofukuta

Kansela Angela Merkel na Rais Barack Obama
Kansela Angela Merkel na Rais Barack ObamaPicha: Getty Images

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anaanza ziara leo ( 01.05.2014)nchini Marekani ambako anatarajiwa kukutana na rais wa nchi hiyo, Barack Obama. Katika ziara yake hiyo inayoanza leo hadi kesho Ijumaa, mzozo wa Ukraine unaofukuta utasaidia kufifisha kashfa ya kunaswa mawasiliano ya simu na kansela huyo kulikofanywa na shirika la usalama wa kitafa la Marekani, NSA.

Wakati uhusiano kati ya Urusi na mataifa tajiri ya magharibi haujawahi kuwa mbaya kama ulivyo tangu vita baridi, viongozi wa siasa na wataalamu wafikiria kuwa mzozo wa Ukraine utawafanya kuwa na msimamo mmoja baada ya miezi 6 ya mkwaruzano.

Hoja zitakazo jadiliwa na viongozi hao wawili ni mkakati wa kumshinikiza rais Vladimir Putin wa Urusi, na mkataba wa ushirikiano katika nchi za magharibi ambao umekuwa ukijadiliwa kati ya marekani na Jumuia ya Umoja wa Ulaya, alisema mshauri wa Kansela Merkel

Hii ni ziara ya kwanza ya bi Angela Merkel Washington tangu aliye kuwa mfanyakazi wa idara ya upelelezi ya Marekani Edward Snowden kutangaza kuwa kituo cha uchunguzi wa data za eletroniki cha Marekani, kimekuwa kikinasa mawasiliano ya simu Ujerumani na hususan simu ya kiganjani ya kansela.

Kadhia ya kusikilizwa simu ya kiganjani ya Merkel na NSA bado ni suala tetePicha: picture-alliance/dpa

Msemaji wa serikali ya Ujerumani, Steffen Seibert, alisema hakuna hatua ilopigwa kuhusiana na mkataba wa kupiga marufuku upelelezi wa pande hizo mbili kama ilivyo kuwa ikipendelea Berlin.

Marekani haipendelei kuwepo na makubaliano ya aina hiyo, kwa hofu ya nchi nyingine kufuata mfano wa Ujerumani.

Kwa mujibu wa gazeti la Der Spiegel, umuhimu juu ya mzozo wa Ukraine utapelekea Angel Merkel kuficha kushindwa kupatikana makubaliano hayo. "

Kutokana na kuzidi kuzorota hali ya Ukraine, mkutano kati ya Merkel na Obama utafikia mkataba wa ushirikiano kati ya nchi za magharibi usiyo na nguvu, wakati " tofauti za kina zikiwepo ". liliandika gazeti hilo.

Hata hivyo "utawala wa marekani utafanya vizuri ikiwa hautofikiria kuwa bi Merkel ameifuta kadhia hiyo", alisema Frances Burnelles mtaalamu wa maswala ya uhusiano katika nchi za magharibi.

" Kama Ukraine yadhihirisha umuhimu wa Marekani na ulaya kushirikiana vizuri na kusahau kashfa ya kunaswa mawasiliano, ni muhimu kwanza kushughulikia maswala hayo na kuyapatia majibu" aliongeza kusema.

Kulia ni Rais wa Urusi Vladmir PutinPicha: EPA/ALEXEY NIKOLSKY / GOVERNMENT PRESS SERVICE

Angela Merkel atawasili washington Alhamisi na atakutana na Obama katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na kuchangia chakula.

Pia atahutubia bodi ya biashara ya marekani na atakuwa na mazungumzo na Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la fedha IMF bi Christine Lagarde na maseneti wa marekani.

Akiwa pamoja na kiongozi wa IMF, watajadili juu ya msaada wa kifedha wanao kusudia kuipatia Ukraine kulipa deni kubwa la nishati kwa Urusi.

" Kansela alokulia Ujerumani ya kikomunisti na Obama ni viongozi wawili wa kisiasa wayakinifu, ambao uhusiano kibinafsi kwanza ni kwa kutumikia ushirikiano wa kimagharibi, na hasa wakati huu wa mgogoro", alisema Mac Kerron mkuu wa ofisi ya fuko la Ujerumani mjini Berlin.

Muandishi/ Amida ISSA

Muhariri/Josephat Charo

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW