1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Angola kuongoza juhudi za upatanishi kati ya Rwanda na DRC

16 Mei 2024

Afisa mkuu wa Marekani amesema nchi ya Angola inafanya kazi ya kuwaleta pamoja viongozi wa Rwanda Paul Kagame na yule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi kutokana na kuongezeka kwa mvutano.

Rais wa Angola Joao Lourenco
Rais wa Angola Joao Lourenco Picha: Adrian Dennis/AFP/AP/picture alliance

Afisa mkuu wa Marekani amesema nchi ya Angola inafanya kazi ya kuwaleta pamoja viongozi wa Rwanda Paul Kagame na yule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi kutokana na kuongezeka kwa mvutano baada ya shambulio la Mei 3 kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani.

Molly Phee, mwanadiplomasia mkuu wa Marekani anayehusika na bara la Afrika, amekiambia kikao cha Bunge hapo jana kuwa Rais wa Angola Joao Lourenco anajaribu kuwaleta pamoja viongozi hao wawili ili kuzifanyia kazi hatua ambazo zimeamuliwa na Marekani na viongozi wa kikanda.

Angola yaongoza mkutano wa kufufua juhudi za amani DRC

Phee amesema Marekani imedhamiria kuendelea na mikakati ya kujaribu kupunguza madhila huko mashariki mwa DRC. Angola, ambayo ni mshirika wa Washington imekuwa pia ikiongoza harakati za kidiplomasia katika lengo la kumaliza miaka mingi ya ukosefu wa utulivu nchini Kongo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW