1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAngola

Serikali ya Angola inazidi kushambulia demokrasia

4 Julai 2024

Serikali ya Angola inalaumiwa na wanaharakati kwa kuendelea kuyakiuka maadili ya kidemokrasia na wamemtaka rais wa nchi hiyo Joao Lourenco aubadilishe mwelekeo huo. Jee wanaharakti hao watafanikiwa.

Maandamano Angola
Maandamano mjini Luanda ya kupinga kuhukumiwa kwa wanaharakati wanne (Septemba): "Uhuru kwa Tanaice Neutro"Picha: Julio Pacheco Ntela/AFP

Mwanaharakati Florindo Chivucute ametoa mwito kwa Rais Joao Lourenco wa kuendeleza demokrasia nchini Angola kwa manufaa ya watu wote wa nchi hiyo. Katika mwito huo mwanaharakati Chivucute amesema rais Joao anapaswa kuubadilisha mwelekeo wa nchi na kwamba hawezi kuendelea kuongoza kama jinsi ilivyokuwa mnamo miaka iliyopita.

Soma pia: Upinzani Angola wawasilisha shauri kupinga matokeo ya urais

Inapasa rais huyo apitie katika njia nyingine. Amesema mwanaharati huyo anayeongoza asasi inayoitwa marafiki wa Angola yenye makao yake mjini Washington. Chivucute ni mwanaharakati na mwanablogu aliyesomea nchini Marekani taaluma ya uchambuzi wa migogoro na utatuzi wake.

Mwanaharakati Tanaice Neutro katika maandamano huko Luanda (mwezi Septemba): hayuko hali nzuri kiafyaPicha: José Adalberto/DW

Mwanaharakati huyo ameelezea wasiwasi wake juu ya hali ya demokrasia nchini Angola. Chivucute anamtaka rais wa Angola kuacha mara moja sera ya kukandamiza demokrasia na haki za msingi. Amesea hatua ya kwanza, ni kutekeleza haki za kiraia kwa kuwaachia wafungwa wote wa kisiasa. "Mheshimiwa Rais, ikiwa kweli unataka nchi ya kidemokrasia na inayoweza kuwanufaisha Waangola wote, huwezi kuendelea kuitawala nchi kama hapo awali! Badilika, hauko kwenye njia sawa! Kuminywa mara kwa mara kwa haki za msingi za kidemokrasia kunamaanisha hatari kwa nchi ya Angola na Waangola."

Soma pia: Blinken kumaliza ziara yake ya ushawishi Afrika huko Angola

Pia amesema pana ulazima wa kuacha sera ya kuwaandama wanasiasa wa upinzani. Jee mwito wa mwanaharakati huyo utasikilizwa?

Serikali ya Angola imekanusha kuwepo wafungwa wa kisiasa nchini. Lakini mashirika ya kutetea haki za binadamu kwa muda mrefu yamekuwa yakilalamika kwamba raia wanaotoa maoni ya kuikosoa serikali, wanabaguliwa, wanakandamizwa na hata wanateswa.

Rais Lourenço: Kuongezeka kwa visa vya watu kukamatwa kiholela?Picha: Issoouf Sanogo/AFP/Getty Images

Mfano ni mkasa wa vijana wanne waliohukumiwa kwenda jela mwaka uliopita.Wanaharakati hao walishiriki kwenye maandamano ya kuwaunga mkono madereva wa teksi waliokuwa wanapinga kupandishwa bei ya petroli. Na tangu wakati huo vijana hao bado wanatumikia vifungo.

Mashirika mbalimbali ya kiraia pamoja na ndugu wa wanaharakati hao wanasema hukumu hiyo imetokana na sababu za kisiasa. Sauti zinazidi kusikika za watu wanaotaka vijana hao wanne waachiwe mara moja. Mashirika hayo na ndugu wa wanaharakati wanasubiri kuona mafanikio ya rufani  iliyowasilishwa.Wanaharakati wamesema waliokamatwa kiholela lazima waachiwe mara moja.

Kwa mujibu wa taarifa kamatakamata sasa imekuwa jambo la kawaida nchini Angola na kwamba hali hiyo imezidi kuwa mbaya tangu rais Joao Laurenco alipoanza kutumikia muhula wa pili. Mashirika ya wanaharakati yameripoti kuwa vijana wengine kadhaa walikamatwa hivi karibuni nchini Angola.

Jengo la Bunge mjini Luanda linadhibitiwa na chama cha Lourenco cha MPLAPicha: Ampe Rogerio/AFP/Getty Images

Kampeni ya serikali dhidi ya mashirika ya kutetea haki za binadamu inazidi kuimarishwa. Na kana kwamba hayo hayatoshi, serikali imepitisha sheria inayoyalenga mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Lengo la sheria hiyo ni kuyaandamana mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoorodhesha mikasa ya watu wanaondamwa kisiasa. Asasi kadhaa zinahofia kuandamwa ikiwa sheria hiyo itaanza kutumika nchini Angola.

Pana hofu kubwa huenda mashirika hayo yakanyamazishwa. Chama cha rais Lourenco MPLA, ambacho kinadhibiti bunge kimeweza kuwasilisha mswada wa sheria hiyo bungeni. Kulingana na sheria hiyo mashirika yote yasiyo ya kiserikali yatatakiwa kutoa taarifa zote juu ya shuhguli zao na jinsi yanavyojiendesha kifedha kwa kisingizio kwamba serikali inawalenga mafisadi na wale wanaotakatisha fedha.

Hatua kwa hatua rais Lourenco anawanyamazisha watu wanaoukosoa utawala wake ili kuyatekeleza maslahi ya chama chake cha kisiasa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW