1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Angola yaituhumu M23 kwa kukiuka usitishaji mapigano Kongo

23 Oktoba 2024

Angola imewatuhumu waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

DR Congo Kibumba 2022 | waasi wa M23
Waasi wa M23 wakiwa na silaha zao huko Kibumba, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Desemba. 23, 2022.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Taarifa iliyochapishwa wiki hii na serikali ya Angola imesema udhibiti wa mji wa Kalembe Jumapili iliyopita na vikosi vya M23 ni ukiukaji wa wazi wa mpango wa usitishaji mapigano. Taarifa hiyo iliongeza kuwa serikali ya Angola inapinga na inalaani vikali kitendo hicho cha uhasama, ambacho kinakiuka juhudi zinazoendelea za kutafuta suluhisho la kudumu kwa mzozo huo. Makubaliano ya kuweka chini silaha kati ya Kongo na waasi wa M23yamekuwepo tangu mapema Agosti kufuatia mchakato wa upatanishi uliosimamiwa na Angola. Lakini makabialiano Jumapili kati ya M23 na wapinagaji wanaoiunga mkono serikali wakijiita Wazalendo katika mji wa Kalembe wa mkoa wa Kivu Kaskazini yalivunja mpango huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW