ANKARA: Kiongozi wa Uturuki Erdogan ziarani Marekani
5 Novemba 2007Matangazo
Waasi wa Kikurd,kaskazini mwa Irak wamewaachilia huru wanajeshi 8 wa Kituruki waliokamatwa wakati wa mapigano ya majuma mawili yaliyopota.Hatua hiyo imechukuliwa siku moja baada ya serikali ya Irak kuapa kuwa itachukua hatua dhidi ya waasi wanaoishambulia Uturuki kutoka kaskazini mwa Irak.
Kwa upande mwingine,Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan hii leo atakutana na Rais wa Marekani George W.Bush mjini Washington.Erdogan amesema,anataka kuona mpango wenye hatua kamili za kukabiliana na wanamgambo wa chama cha Kikurd cha PKK kaskazini mwa Irak.Uturuki imetishia kuchukua hatua ya kijeshi ikiwa waasi hao hawatositisha mashambulizi yao.